top of page
Search

Untitled

NI JUKUMU LETU SOTE

Siku za hivi karibuni nimekuwa nikisoma historia ya mtume Muhammad, pamoja na biblia mara kwa mara. Japo kuna mengi sana ya kujifunza kwenye hivi vitabu, mtume Muhammad na Yesu walikuwa na moja linalofanana, wote walichukua jukumu la kuzibadilisha jamii walizokuwa wanaishi. Mtume Muhammad akiwa kijana mdogo anayemsaidia biashara mjomba wake, aliyaona machafu yanayoendelea kwenye mji wa Mecca; kama kuabudu sanamu, kuamini miungu nk., aliamua kwa dhati kuanza kuhubiri habari ya Mungu mmoja ili kuirekebisha jamii. Yesu akiwa bado kijana mdogo, aliingia kwenye hekalu na kuleta vurugu baada ya kuona nyumba ya baba yake inageuzwa kuwa pango la wanyang’anyi. Hawa wote waliongozwa na lengo moja tu; walitamani kuibadili na kuifanya jamii kuwa bora kwa kutangaza habari za Mungu mmoja.

Baada ya kujifunza hili, nikajiuliza hivi kwa nini na sisi kwa umoja wetu tusifanye jambo? Tuna changamoto kibao kwenye jamii yetu, nyingi zikisababishwa na umaskini uliokithiri. Tukiweza kuunganisha nguvu zetu na kuhamasishana, pengine neno moja, ushauri au nasaha yako;

  1. Ingemuamsha yule kijana alizama au anayeelekea kuzama kwenye dimbwi la madawa ya kulevya kwa kushindwa kutambua ndoto zake.

  2. Pengine nasaha/ushauri wako ungemfumbua macho yule kijana aliyekata tamaa na kuamua kuwa mlevi wa kupindukia.

  3. Pengine hamasa yako ingemtia moyo yule dada aliyekata tamaa na kuamua kufanya biashara ya kuuza mwili.

  4. Pengine maneno yako yangemhamasisha yule mwanafunzi aliyeacha shule kwa sababu ya kubeba mimba.

  5. Pengine maarifa yako yangembadilisha yule kijana mwenye nguvu aliyeamua kuwa kibaka na mwizi.

  6. Pengine kwa mawazo yako, wote tungegundua tunapokosea na kujirekebisha mapema kabla hatujapotea kabisa.

Haya ni mambo ambayo tunaweza kuyafanya wenyewe bila gharama yoyote. Tutakapokuwa kwenye jamii bora, tunakuwa na mazingira rafiki ya kuzifikia ndoto zetu lakini pia mazingira salama ya kulea watoto wetu na wadogo zetu. Katika Safari ya ndoto zetu, tunahitaji pia kujengana; kushauriana na kuhamasishana. Safari ni ngumu, kuna wenye uwezo wana kuvumilia wenyewe na kuna wengine wanahitaji kuvutwa, itapendeza sana kama siku moja tutafurahi pamoja.

Miaka kumi ijayo tutakuwa watu wengine tofauti kabisa; itatufanya tujisikie vizuri mtu akitushukuru kwa kusema “ahsante kwakuwa ulisema neno hili/ulinipa ushauri huu ukabadilisha maisha yangu.”

IPIGANIE NDOTO YAKO; IPAMBANIE NDOTO YAKO

WEWE NI MSHINDI

 
 
 

Recent Posts

See All
JE KUNA BAHATI KATIKA MAISHA?

JE KUNA BAHATI KATIKA MAISHA? Oprah Winfrey aliwahi kusema, hakuna bahati kwenye maisha wala hakuna anayefanikiwa kwa kubahatisha....

 
 
 
ANZA NA KIDOGO

KITUMIE KIDOGO ULICHONACHO; MUNGU ATAKUONGEZEA MBELE YA SAFARI Wengi wetu huwa tunazidiwa na hofu na kuogopa kuanza kutembea kuelekea...

 
 
 

Comments


Post: Blog2_Post

Subscribe Form

Thanks for submitting!

  • Facebook
  • Twitter
  • LinkedIn
  • Facebook

©2020 by Maabara Ya Maisha. Proudly created with Wix.com

bottom of page