top of page
Search

ANZA NA WEWE

Siku moja rafiki yangu John alikuwa anasafiri na gari ya rafiki yake kutoka Tanga kuelekea Mafinga. John alichukua gari kwa jamaa usiku akalala nayo kwake ili aanze Safari mapema. Asubuhi na mapema John akawasha gari na kuanza Safari. Kabla hajaondoka mjini, akapita sheli akajaza mafuta kisha akaondoka. Baada ya umbali fulani gari ikaanza kuzingua, mwisho ikazima kabisa. John alikasirika kwasababu alikuwa na haraka. Akiwa ndani ya gari akaanza kulaumu “mgari gani wa kimaskini huu; mgari unazima zima; angalia maviti yalivyochoka” nk. John alikasirika sana, akapiga piga sterling, piga ngumi kwenye dashboard lakini haikusaidia. John alipiga starter mpaka akachoka lakini gari haikuwaka. Akaamua kutoka nje ya gari akiwa na hasira kibao. Baada ya kufungua mlango tu kuna gari nyingine ikapita kwa kasi na kukanyaga maji yaliyokuwa yametuama barabarani; yote yakamwogesha John. Alizidi kukasirika hasira machozi yakawa yanamtoka. Akaanza kulaumu gari; akalaumu ubovu wa barabara, akamlaumu yule aliyekanyaga maji yakamwagikia, akaanza pia na kumlaumu rafiki yake aliyemuazima gari. Wakati akiwa katikati ya manung’uniko ikapita gari nyingine ikipiga honi kwanguvu; John alikasirika zaidi. Akaanza kuipiga gari yake Mateke na mangumi mpaka akaumia vidole na mguu. Baada ya kukaa masaa mawili bila kujua chakufanya, mwisho alinyanyua simu na kumpigia fundi. Fundi alipofika alimuhoji John maswali kama vile kwanini imezima? Ulikagua gari asubuhi kabla haujaanza Safari? Uliongeza maji/coolant? Ulipima oil ya engine? Na mengine kibao. Kisha fundi akafungua boneti akaongeza maji, kagusa gusa nyaya, kaweka betri vizuri na mambo mengine machache. Baada ya hapo John akawasha gari mara moja ikawaka. Fundi akadai fedha yake kisha akamwambia John siku nyingine kabla haujaanza Safari, hakikisha unakagua gari kwanza na kufanya vya muhimu kama kuongeza maji, oil nk. Baada ya hapo John akaendelea na Safari muda akiwa makini kuangalia geji kila mara lakini pia vidole na mguu wake ukiwa na maumivu makali.

Ujumbe

Bwana John hana tofauti sana na sisi katika Safari ya mafanikio. Tunapokutana na changamoto, huwa ni wepesi sana kulaumu watu, kulaumu hali ya hewa, kulaumu mazingira, kumlaumu mwajiri, kulaumu serekali, kulaumu elimu na wakati mwingine kulaumu umaskini wa wazazi wetu nk. Lakini, ni mara chache sana huwa tunajilaumu wenyewe, mara chache sana huwa tunajiuliza je, nilikagua gari kabla kuanza Safari? Tafiti zinaonesha moja ya tabia sugu za watu wasiokuwa na mafanikio ni kulaumu watu wengine bila wao wenyewe kujitathmini. Pengine changamoto unayokutana nayo ni kwasababu haukufanya maamuzi fulani sahihi; pengine ulilimbikiza deni ambalo lilikuwa dogo mpaka likafikia mahali likakushinda ndio maana nyumba imeuzwa; pengine haukuweka mbolea na kupiga dawa kwa wakati mazao yako ndio maana mavuno mabaya; pengine ulipoteza uaminifu ndio maana watu wanashindwa kukukopesha; pengine umekuwa mchafu sana ndio maana wateja hawaji kwenye mgahawa wako; pengine umekuwa mlevi sana ndio maana umepoteza marafiki; pengine unatumia muda mwingi sana kwenye mambo yasiyokuwa ya msingi ndio biashara yako na kazi zako zinasua sua; pengine unaongea sana kuliko kutenda ndio maana ndoto yako inachelewa; pengine una washauri wabaya ndio maana haupigi hatua nk.

Natambua kuna changamoto ambazo zipo juu ya uwezo wetu lakini changamoto nyingi huwa zinakuja kutokana na baadhi ya maamuzi yetu tuliyowahi na tunayoendelea kuyafanya. Na bahati mbaya, tunapotumia muda mwingi kunyooshea watu wengine vidole na kulaumu kila kitu bila kujigusa sisi, tunapunguza uwezekano wa kutatua hiyo changamoto kwasababu hatutaki kutafiti kiini cha hiyo changamoto. Muda lioutumia John kulalamika, kualaumu, kupigapiga pengine angeutumia kujiuliza maswali angegundua kuwa hakukagua gari wakati anaanza safari.

Kuanzia leo, tukikutana na changamoto yoyote, tuanze kwanza kwa kujiangalia na kurekebisha yale tuliyokosea na yale yaliyopo kwenye uwezo wetu. Kwa kujiwajibisha kwa mapungufu yetu, tutakuwa tunajiweka kwenye hatua nzuri zaidi ya kuzifikia ndoto zetu. Ukikutana na changamoto, tumia muda mwingi kutafuta utatuzi kuliko kulaumu. Jiwajibishe mwenyewe kwa mambo unayokutana nayo kwenye maisha yako badala ya kunyooshea watu wengine vidole.

IPIGANIE NDOTO YAKO; PAMBANIA NDOTO YAKO

WEWE NI MSHINDI.

Onesmo Mushi

 
 
 

Recent Posts

See All
JE KUNA BAHATI KATIKA MAISHA?

JE KUNA BAHATI KATIKA MAISHA? Oprah Winfrey aliwahi kusema, hakuna bahati kwenye maisha wala hakuna anayefanikiwa kwa kubahatisha....

 
 
 
ANZA NA KIDOGO

KITUMIE KIDOGO ULICHONACHO; MUNGU ATAKUONGEZEA MBELE YA SAFARI Wengi wetu huwa tunazidiwa na hofu na kuogopa kuanza kutembea kuelekea...

 
 
 

Comments


Post: Blog2_Post

Subscribe Form

Thanks for submitting!

  • Facebook
  • Twitter
  • LinkedIn
  • Facebook

©2020 by Maabara Ya Maisha. Proudly created with Wix.com

bottom of page