top of page
Search

HAKUNA MAAMUZI MADOGO KWENYE MAISHA

Kuna kijana mmoja anaitwa Dominic alikopa fedha bank kiasi cha shilingi milion 15 ili aweze kufungua biashara. Dominic alikuwa amedhamiria kujikwamua, alikuwa ana mawazo ya tija kiasi kwamba akikusimulia unatamani kuungana naye. Kwakuwa biashara ilikuwa haijaanza, Dominic akaamua kuiweka pesa yake bank ili aendelee kutafuta eneo zuri la kufanyia biashara yake. Mwezi wa kwanza ukapita, mwezi wa pili katikati, mpenzi wake aliyekuwa anasoma chuo akamtembelea akakuta Dominic hana chochote ndani zaidi kitanda chake. Dada akamshangaa kweli Dominic, “Dommy jamani, yani hata kochi umeshindwa kununua?” Dominic akaona asimkwaze mpenzi wake, akajisemea “Nina milioni 15, nikitoa laki tatu nikanunua masofa haitaharibu chochote.” Basi Dominic akatoka siku iliyofuata akaenda kununua masofa. Alipoyaweka ndani, daaah pakavutia sana ila sakafu ikaharibu show. Dominic akasema aahhh, nikitoa laki moja nikanunua carpet patavutia zaidi lakini pia sio hela nyingi. Basi Dominic akatoka akaenda kununua carpet, alipofika dukani badala ya kununua la laki, akanunua carpet la manyoya la laki mbili lililokuwa na muonekano mzuri zaidi. Kweli nyumba ilipendeza sana ila aahhh, Dominic akaona upweke kukaa bila TV basi akajisemea “naenda kununua TV tu basi kila kitu kitakuwa kimekamilika.” Looh Dommy akavutiwa na TV za kisasa pale dukani mwisho akashawishiwa na muuzaji kuwa kwasababu anapenda kuangalia mpira, TV kubwa itamfaa. Basi Dommy akanunua TV kubwa ya Sonny inch 63 kwa shilingi laki saba. Alipoiweka ndani, aisee hakuwa hata anataka kutoka nje. Lakini pakawa na tatizo moja, TV haikuwa na Meza kwahiyo ikawa haivutii kiasi kile. Dommy akajisemea “hivi nikianza biashara nikapiga mishe hizi na zile si dakika tu nimerudi ana hii hela tena ukizingatia Nina mtaji wa nguvu?” Dommy akatoka akaenda kununua meza nzuri kabisa ya kisasa inayoendana na ile TV. Mambo yakawa mswano nyumba inapendeza, Dommy akajisemea wacha nikamilishe kabisa ninunue king’amuzi ili niangalie mpira, bank bado hela ipo nyingi tu. Baada ya vitu vyote hivi kujaa ndani, ikaja changamoto moja, Dommy akaona nyumba anayokaa ni ndogo na haiendani na hadhi ya vitu alivyokuwa navyo ndani. Dommy akaamua kuhama pale, akapanga nyumba kubwa yenye vyumba viwili, jiko, seating room kubwa safi kabisa kwa shilingi laki mbili kwa mwezi. Maisha yakamnyookea Dommy nyumba ikawa inapendeza. Dommy akanunua fridge kubwa na jiko zuri kabisa la gesi. Baada ya miezi michache Dommy akabadilisha aina ya maisha ya kujibana aliyokuwa anaishi mwanzo, akajisemea “biashara nitakayofunguwa itanilipa sana, si unamuona fulani na fulani?” Dommy akajiambia ili niweze kuzungukia maeneo vizuri na kukagua kwa ajili ya biashara yangu inabidi nipate kausafiri, basi Dommy akanunua pikipiki aina ya Boxer, yes, mambo yakawa yanaenda vizuri kabisa. Dommy akaja kupata eneo la kufanyia ile biashara yake lakini mtaji ukawa umepungua sana. Mara ya mwisho nakutana naye alinimbia kuna mishe anafanya ili ajazie mtaji, ila kuna rafiki yake wa karibu amenijuza kuwa Dommy hajaanza ile biashara mpaka leo japo miezi karibu kumi imeshapita.


KWA KUMBUKUMBU YANGU, DOMMY ALIANZA NA SOFA TU.


Kupanga ni kuchagua!!!!!!

💪💪💪💪💪💪💪💪💪💪💪💪💪💪

 
 
 

Recent Posts

See All
JE KUNA BAHATI KATIKA MAISHA?

JE KUNA BAHATI KATIKA MAISHA? Oprah Winfrey aliwahi kusema, hakuna bahati kwenye maisha wala hakuna anayefanikiwa kwa kubahatisha....

 
 
 
ANZA NA KIDOGO

KITUMIE KIDOGO ULICHONACHO; MUNGU ATAKUONGEZEA MBELE YA SAFARI Wengi wetu huwa tunazidiwa na hofu na kuogopa kuanza kutembea kuelekea...

 
 
 
Kama unavyotafuta hewa

KAMA UNAVYOTAFUTA HEWA Kuna bwana mdogo mmoja alikuwa anatamani sana kufanikiwa katika maisha yake ila hakujua apambane kiasi gani. Siku...

 
 
 

Comments


Post: Blog2_Post

Subscribe Form

Thanks for submitting!

  • Facebook
  • Twitter
  • LinkedIn
  • Facebook

©2020 by Maabara Ya Maisha. Proudly created with Wix.com

bottom of page