top of page
Search

JE KUNA BAHATI KATIKA MAISHA?

JE KUNA BAHATI KATIKA MAISHA?

Oprah Winfrey aliwahi kusema, hakuna bahati kwenye maisha wala hakuna anayefanikiwa kwa kubahatisha. Aliendelea kusema tunachokiita bahati mara nyingi ni juhudi na maandilizi ya mtu binafsi yanakutana na fursa. Mimi nakubaliana naye kwa asimilia mia moja.

Lakini pia biblia yangu hakuna mahali imetaja neno “bahati” au hata kulizungumzia. Kuna uwezekano lipo sehemu sijaliona maana sina utaalamu wa theolojia.


Binafsi naamini, kutimiza malengo ya maisha yetu ni matokeo ya kujituma kwetu, kukitumia kwa ufasaha na nguvu zote kile Mungu alichokiweka ndani yetu. Biblia yangu inaniambia kwenye Wagalatia 6:7, kila mwanadamu atavuna alichokipanda. Kwa uelewa wangu hapa, ukipanda juhudi utavuna maradufu sawasawa na juhudi zako na vivyo hivyo ukipanda uvivu na kutokuwajibika “ipasavyo” utavuna kiduchu au wakati mwingine usivune kabisa.

Lakini biblia yangu haisemi upande tu halafu usubiri kuvuna, bali ukitunze ulichokipanda ili uweze kuvuna. Kitabu cha Mhubiri 11:6-7 inasema panda mbegu yako asubuhi na jioni na jioni usiiache mikono yako ikakaa bila la kufanya.

Lakini pia ukisoma hadithi za mtume, kuna muda alikuwa jangwani. Moja ya maswahaba wake akamwambia mtume, mimi namuacha ngamia wangu azungukezunguke tu Mungu atamlinda. Mtume alimjibu, hapana, mfunge ngamia wako kwanza kisha mwachie Mungu amlinde. Nadhani mtume alimaanisha, ni lazima kwanza wewe ucheze nafasi yako kisha umuachie Mungu.


Kwa uelewa wangu mdogo, maisha yanahitaji zaidi juhudi na maarifa ya kufanikisha jambo fulani. Mafanikio yanakuja kutika kuwajibika, hakuna bahati wala muujiza.


Ni mawazo yangu, unaweza kunipinga.🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿

 
 
 

Recent Posts

See All
ANZA NA KIDOGO

KITUMIE KIDOGO ULICHONACHO; MUNGU ATAKUONGEZEA MBELE YA SAFARI Wengi wetu huwa tunazidiwa na hofu na kuogopa kuanza kutembea kuelekea...

 
 
 
Kama unavyotafuta hewa

KAMA UNAVYOTAFUTA HEWA Kuna bwana mdogo mmoja alikuwa anatamani sana kufanikiwa katika maisha yake ila hakujua apambane kiasi gani. Siku...

 
 
 

Commentaires


Post: Blog2_Post

Subscribe Form

Thanks for submitting!

  • Facebook
  • Twitter
  • LinkedIn
  • Facebook

©2020 by Maabara Ya Maisha. Proudly created with Wix.com

bottom of page