
Je ukifa leo?
- Onesmo Frank
- May 18, 2020
- 1 min read
Kama ukifa leo, ni ndoto gani zitakufa na wewe? Ni matamanio gani makubwa ambayo yangeweza kuibadilisha jamii yetu lakini uliogopa kuyapigania kwasababu ya hofu? Ni jambo gani utajilaumu nalo ukiwa pale kitandani na kusema “ningejua, ningetekeleza hili?”.
Ni wizi na unyang’anyi mkubwa tutakuwa tumeufanya kwa watoto wetu, wajukuu na vitukuu vyetu, kama hatutoota na kuziishi ndoto zetu. Maisha tunayoyaishi sasa, matibabu tunayoyapata, teknolojia tunayoifurahia, ndege, meli, treni na magari tunayoyapanda, michezo tunayoiangalia, vitabu tunavyovisoma, movie tunazofurahia, muziki tunaosikiliza, mahubiri tunayoyapokea, barabara, na majumba tunayoishi, vyote ni matokeo ya ndoto za watu ambazo baadhi ya watu walizishinda hofu zao na kuamua kuzipigania.
Je itakuwa rahisi? Hapana. Nelson Mandela alifungwa miaka 27 kwa kuipigania ndoto yake, Mwalimu Nyerere alikubali kuishi maisha ya kimaskini ili kuipigania ndoto yake, Mahtma Gandhi aliridhia kujinyima chakula na kufunga kwa njaa na kuhatarisha maisha yake ili kuipigania ndoto yake, Yesu mwana wa Mungu alikubali kuteswa na kufa kifo cha aibu kuliko vyote duniani ili tu kuikamilisha ndoto, Mtume Muhammad alitukanwa, akapigwa, akafedheheshwa akakubali kuyapitia yote ila kuikamilisha ndoto yake. Haitokuwa rahisi lakini inawezekana.
Unapokubali kuipigania ndoto yako, umekubali kupambana kuibadilisha jamii yako. Usikubali kuondoka hapa duniani bila kuikamilisha ndoto yako. Wala usiogope kwakuwa Penye nia pana njia.
Onesmo Mushi.
https://onesmofrenk.wixsite.com/website
https://www.facebook.com/PIGANIANDOTOYAKO
Comments