top of page
Search

Tuweke akiba

Kesho itakuwaje?

Kwa mama aliye mjamzito sasa, miaka kumi ijayo mtoto atakuwa darasa la tano. Mwenye Miaka 40 sasa hivi atakuwa tayari kwenye kundi la wazee, na mwenye miaka 30 atakuwa kwenye makamo. Wengi wetu tutakuwa tumeongeza familia mara dufu, na majukumu nayo yatakuwa yamekolea. Kwasababu, mtoto aliyepo shule ya msingi darasa la nne leo, atakuwa chuo kikuu Mungu akijalia. Kwahiyo kama una watoto wawili au watatu, jumlisha wazazi wako ambao watakuwa wamezeeka wanakutegemea, unaweza kuiona vizuri picha ya kesho.

Ndugu zangu, embu tuzungumze kidogo kuhusu pesa. Naamini kila mmoja wetu anafahamu kuwa kadri umri unavyozidi kusogea, ndio mambo yanavyozidi kuwa magumu. Na kama bado haujaamua kubadilika, ndio yanakuwa magumu kabisa. Halafu hapa ni vijana wenye nguvu mambo yapo hivi, tukifika miaka 40 na 50 nguvu zimeanza kuisha itakuwaje? Vipi watoto wetu? Vipi maisha yetu ya uzee? Hivi wote tutakubali kuwa ombaomba kweli?

Nataka kukushawishi jambo, embu kuanzia leo tujifunze kuwekeza kwenye kesho yetu. Tujifunze kuweka akiba ya kesho haijalishi ni kidogo kiasi gani. Ukiweza kujiwekea shilingi mia mbili tu (200) kwa siku, ambayo naamini nimemgusa yule wa chini kabisa, kwa Mwaka ni shilingi 73,000. Kwa miaka kumi ni 730,000 (laki saba na elfu thelathini). Kama unaweza kuweka shilingi 500 kila siku kwa ajili ya kesho yako, kwa Mwaka utakuwa na 182,500 (laki moja na elfu themanini na mbili na mia tano) na kwa miaka kumi ni karibu milioni mbili.

Hii shilingi mia mbili au mia tano unayoitunza kila siku inaweza kukuokoa na mengi sana. Hii mia mbili itamsaidia mwanao aende shule bila wewe kulazimika kwenda kukopa, hii mia tano inaweza kukusaidia kabiashara pale nguvu zitakapokuwa zimeisha.

Embu tujaribuni wapendwa, inawezekana kabisa wala usidharau. Kiasi chochote kila unachoweza kukitunza kila siku, jaribu kutunza kuna siku utaona faida yake. Nilichojifunza kwa wenzetu nchi zilizoendelea, karibu kila mtu ana account yake ya uzeeni. Kila siku wanatunza kiasi fulani kidogo kabisa cha pesa ndio maana utawaona watalii wengi ni wazee wazee. Ni kwasababu, walikusanya fedha za kuuishi uzee wao.

Kila siku ukipata pesa, kabla haujaifanyia chochote kile, anza kwa kujilipa kwanza. Jilipe kwasababu ya maisha yako ya kesho.

Najua kipato ni kidogo sana lakini embu kwa siku mbili karibu kuandika kila shilingi unayoitumia kuanzia asubuhi mpaka jioni kisha jiulize ni matumizi mangapi umeyafanya ambayo sio ya msingi. Kama ni mvuta sigara, unaweza kupunguza sigara moja tu ukaweka hiyo mia mbili. Badala ya kunywa soda mbili, unaweza kunywa moja, moja ukasave. Kwa mlevi, ukipunguza bia moja tu kwa wiki, unaweza kusave shilingi 500 karibu kila siku. Badala ya kula kwa mama ntilie elfu 2000 mchana na 2000 jioni, unaweza ukabalance nyumbani, ukaweka akiba kinachobaki. Badala ya kula mahindi mawili ya kuchoma, unaweza kula mmoja ukasave hiyo 500.

Kabla haujawanunulia marafiki bia, nyama na chochote, jiulize kwanza kama umeshaweka akiba ya kesho yako.

Weka akiba na usiitumie kwa sababu yoyote ile, kesho utamshukuru Mungu kwa kufanya hivyo. Ndoto zetu zinahitaji nidhamu ya hali ya juu.

TUKIAMUA INAWEZEKANA.💪💪


Onesmo Mushi


https://onesmofrenk.wixsite.com/website

https://www.facebook.com/PIGANIANDOTOYAKO

 
 
 

Recent Posts

See All
JE KUNA BAHATI KATIKA MAISHA?

JE KUNA BAHATI KATIKA MAISHA? Oprah Winfrey aliwahi kusema, hakuna bahati kwenye maisha wala hakuna anayefanikiwa kwa kubahatisha....

 
 
 
ANZA NA KIDOGO

KITUMIE KIDOGO ULICHONACHO; MUNGU ATAKUONGEZEA MBELE YA SAFARI Wengi wetu huwa tunazidiwa na hofu na kuogopa kuanza kutembea kuelekea...

 
 
 

Comments


Post: Blog2_Post

Subscribe Form

Thanks for submitting!

  • Facebook
  • Twitter
  • LinkedIn
  • Facebook

©2020 by Maabara Ya Maisha. Proudly created with Wix.com

bottom of page